Pata taarifa kuu
KENYA-MAANDAMANO-UCHAGUZI

Chebukati: Napanga kukutanisha Kenyatta na Odinga kabla ya uchaguzi wa Oktoba 26

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekutana na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) kabla ya uchaguzi mpya uliopangwa kufanyika siku ya Alhamisi Oktoba 26.

Rais uhuru Kenyatta anasema yuko tayari kwa uchaguzi ujao wa Oktoba 26.
Rais uhuru Kenyatta anasema yuko tayari kwa uchaguzi ujao wa Oktoba 26. ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita Wafula Chebukati alikutana na kiongozi wa muungano wa upinzani Raila Odinga.

Mapema wiki iliyopita Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC aliomba mazungumzo ya moja kwa moja kati ya rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga. Mazungumzo ambayo yalifutiliwa mbali na rais Kenyatta.

Raila Odinga alitangaza kutoshiriki uchaguzi wa Oktoba 26. Lakini baada ya kukutana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, alilegeza msimamo na kusema anaweza kubadilisha mawazo na kurejea kwenye kinyang'anyiro cha kuwania urais iwapo kutakuwa na mazungumzo na kufanyika kwa mageuzi ndani ya Tume ye Uchaguzi.

Awali alitolea wito wafuasi wake kufanya maandamano makubwa siku ya uchaguzi.

Bw. Chebukati ameambia vyombo vya habari kwamba anapanga kuwakutanisha Raila Odinga na Uhuru Kenyatta kabla ya uchaguzi wa mpya urais uliopangwa kufanyika siku ya Alhamisi Oktoba 26.

Makabiliano kati ya wafuasi wa upinzani na vikosi vya usalama yamekua yakishuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini Kenya. Makabiliano hayo yamesababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi kukamatwa.

Mashirika mbalimbali ya haki za binadamu yamekua yakitoa wito wa utulivu na kuvumialiana. Uchaguzi mpya wa urais umepangwa kufanyika Oktoba 26, baada ya Mahakama ya Juu nchini humo kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 8, ambapo Rais Uhuru Kenyatta aiibuka mshindi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.