Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Raila Odinga: Ninatafakari uwezekano wa kushiriki uchaguzi

media Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya, NASA, Raila Odinga. REUTERS/Baz Ratner

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema, anaweza kubadilisha mawazo na kurejea kwenye kinyanganyiro cha kuwania urais iwapo kutakuwa na mazungumzo na kufanyika kwa mageuzi ndani ya Tume ye Uchaguzi.

Odinga ametoa kali hii baada ya kukutana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi jijini Nairobi.

Mkutano huu umekuja baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati hapo jana kuomba mazungumzo ya moja kwa moja kati ya rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.

Hata hivyo, mkutano huo haujafanyika kama ilivyokuwa imepangwa na baada ya Odinga kuzungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, amemwambia kuwa atakutana na rais Kenyatta siku ya Jumatatu.

Uhuru Kenyatta kwa upande wake, akiendelea na kampeni za kisiasa amesema kuwa mazungumzo pekee anayoweza kushiriki ni kuhusu namna Uchaguzi wa wiki ijayo utakavyofanyika kwa amani.

Hii ni dalili kuwa huenda mwafaka usipatikane hivi karibu kuhusu Uchaguzi wa tarehe 26.

Odinga ameitisha maandamano ya nchi nzima siku ya kupiga kura, hali ambayo imeendelea kuzua wasiwasi.

Wachambuzi wa siasa wameendelea kutoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo na kuahirsihwa kwa Uchaguzi huu kwa sababu tayaru Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi amesema, itakuwa ni viumu kuwa na uchaguzi huru na haki katika mazingira haya. Wito kama huu umetolewa na mashirika ya kiraia nchini humo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana