Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Raila Odinga aitisha maandamano Oktoba 26

media Uhuru Kenyatta na Raila Odinga kila mmoja akitoa msimamo wake kuhusu uchaguzia wa Oktoba 26. DR.

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ameitisha maandamano ya nchi nzima tarehe 26, siku ambayo Uchaguzi mpya wa urais umepangwa kufanyika.

Raila Odinga ambaye alijitoa katika Uchaguzi huo amesisitiza kuwa Uchaguzi hauwezi kufanyika bila mabadiliko ndani ya Tume ya Uchaguzi.

Mwenyekiti wa Tume hiyo ya Uchaguzi Wafula Chebukati tayari amesema kuwa anatilia shaka, iwapo uchaguzi huo utakuwa huru na haki iwapo viongozi wa kisiasa nchini humo hawatazungumza na kutatua mzozo wa kisiasa unaoendelea.

Wakati huo huo Rais Uhuru Kenyatta ameitisha maombi kabla ya marudio ya Uchaguzi, licha ya kusema baadaye kuwa hana cha kuzungumza.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa nchi itafanya maombi mwisho wa wiki hii kabla ya marudio ya uchaguzi mkuu wa wiki ijayo.

Taarifa ya Rais Kenyatta ilikuja baada ya afisa wa cheo ya juu kwenye Tume ya Uchaguzi Roselyne Akombe, kukimbia nchi akisema kuwa amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa.

Rais Kenyatta alisema kuwa wakenya watatumia wikendi kwa maombi na maridhiano kabla ya marudio ya uchaguzi wa urais ambao umepangwa kufanyika tarehe 26 mwezi Oktoba.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana