Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 23/09 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 23/09 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 22/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Kampuni kubwa ya kitalii duniani Thomas Cook yafilisika
 • Kanisa Katoliki nchini Burundi laishtumu serikali ya Burundi
 • Chanjo ya pili ya Ebola kuanza kutolewa nchini DRC mwezi Oktoba
E.A.C

Kampuni ya Barrick yakubali kuilipa Tanzania dola za Marekani milioni 300

media Rais John Magufuli (katikati) akitazama utilianaji saini wa makubaliano ya maelewano kati ya Barrick Gold na Serikali ya Tanzania. Octoba 19, 2017 Ikulu/Tanzania

Kampuni ya kimataifa ya uchimbaji madini ya Barrick Gold ambayo hivi karibuni iliingia kwenye mgogoro na Serikali ya Tanzania, imekubali kuilipa Serikali kiasi cha dola za Marekani milioni 300.

Hatua hii imetangazwa Alhamisi hii wakati kamati mbili za majadiliano ile ya Tanzania na ya Barrick zilipokuwa zikiwasilisha ripoti ya mazungumzo yao kwa rais John Pombe Magufuli.

Akizungumza wakati akiwasilisha shukrani za kampuni yao, mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Barrick John Thornton, amesema kampuni yao italipa kiasi cha dola za Marekani milioni 300 kama njia ya kuonesha utayari wake na uaminifu kwa Serikali ya Tanzania.

Thornton amesema licha ya kuwa kwa sehemu kubwa wameafikiana masuala mengi, lakini suala ya tozo ya malimbikizo ya kodi bado hawajakubaliana kikamilifu na kwamba wameliweka kiporo wakati akiwasiliana na wanahisa wengine ili kufikia makubaliano zaidi.

Serikali ya Tanzania mwanzoni mwa mwaka huu ilipiga marufuku kusafirishwa nje ya nchi kwa mchanga wa madini wa kampuni ya Barrick kwa kile ambacho ilisema ni kuwepo kwa udanganyifu kuhusu thamani ya madini yaliyomo kwenye mchanga huo.

Baadae rais Magufuli aliunda kamati mbili kufanya uchunguzi wa mchanga wa madini ambapo zilibaini kuwepo kwa udanganyifu na rushwa wakati wa ujazaji wa nyaraka kuidhinisha mchanga huo kusafirishwa nje ya nchi.

Kwa upande wake rais Magufuli ameushukuru uongozi wa Barrick kwa kuona udhaifu uliokuwepo na kukubaliana na uelekeo mpya wa Serikali yake katika uendeshaji na usimamizi wa migodi nchini humo.

Rais Magufuli amesema "lengo letu lilikuwa ni zuri tu kwamba ni lazima tulinde rasilimali zetu ili ziwanufaishe wananchi na kuwaletea maendeleo kupitia madini".

Aidha kiongozi wa timu kutoka Tanzania ambaye pia ni waziri wa sheria na katiba Profesa Paramagamba Kabudi, amesema mazungumzo yalikuwa magumu na kuna wakati ilifikia kama yanaenda kushindikana lakini baadae waliafikiana na kuendelea mbele.

Paramagamba Kabudi amesema miongoni mwa makubaliano ni pamoja na Serikali kupata hisa za asilimia 16 kwa kila kampuni ya Barrick, faida itakayopatikana kutokana na biashara ya dhahabu sasa utagawanywa sawa kwa sawa kwa maana ya asilimia 50/50 na pia kampuni hiyo kuwa inahifadhi fedha zake kwenye mabenki ya Tanzania.

Katika makubaliano haya pia ambayo yametiwa saini na pande hizo mbili, kampuni ya Barrick imekubali kutekeleza matakwa ya mabadiliko ya sheria za madini yaliyopitishwa na bunge la Tanzania.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana