Pata taarifa kuu
KENYA-IEBC-UCHAGUZI

Mmoja wa maafisa wakuu wa tume ya uchaguzi Kenya ajiuzulu

Kamishna wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu katika tume hiyo, ikiwa zimesalia siku zisizozidi nane kabla ya uchaguzi mpya wa urais ulipangwa kufanyika Oktoba 26.

Maofisa wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, wakiwa katika shughuli ya kuandikisha wapiga kura wapya, 16 Januari 2017.
Maofisa wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, wakiwa katika shughuli ya kuandikisha wapiga kura wapya, 16 Januari 2017. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa aliyoitoa akiwa mjini New York anakoishi, Bi. Akombe amesema kuwa marejeo ya uchaguzi utakaofanyika hayaendani na matarajio ya uchaguzi ulio huru na wa haki.

Dkt Akombe alijiunga na tume ya IEBC baada ya kuhudumu katika Umoja wa Mataifa.

Bi Akombe amesema uamuzi wake wa kujiuzulu katika Tume ya Uchaguzi IEBC utawaudhi baadhi ya maaafisa wengine.

“Nilijaribu kadiri ninavyoweza lakini nimeshindwa kuvumilia. Wakati mwingine, unalazimika kusalimu amri na kujiuzulu, inapofikia maisha ya watu kuwa hatarini," Roselyn Akombe amesema katika taarifa yake.

Uamuzi huu wa Bi Akombe unakuja ikiwa zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Oktoba 26.

Muungano wa upinzani NASA umekua ukiitisha maandamano ya kila siku kushinikiza mageuzi ndani ya Tume ya Uchaguzi, ukishtumu maafisa wa tume hiyo kula njama ya kuiba kura katika uchaguzi wa Agosti 8, ambao matokeo yake yalitenguliwa na Mahakama ya Juu nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.