Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Mbowe: Lissu anaendelea vizuri na huenda akaruhusiwa kuondoka hospitali wiki ijayo

media Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, cha Tundu Lissu, wakiwa kwenye moja ya mikutano ya chama hicho wakati wa kampeni za urais mwaka jana. RFI

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu ameondolewa katika chumba mahututi, na huenda akaruhusiwa kwenda nyumbani wiki ijayo, kwa mujibu watu wa karibu yake.

Chama chake cha CHADEMA, kimesema Lissu anayeendelea kupokea matibabu jijini Nairobi nchini Kenya baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulijana mwezi Septemba, aliondolewa kwenye chumba hicho wiki iliyopita.

Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, amesema Tundu Lissu sasa anaweza kuketi na kula mwenyewe.

Mbowe amewaambia waandishi wa habari kwamba kwa mujibu wa madaktari, hali ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu imeimarika na hivyo wakati wowote kuanzia wiki ijayo anaweza kuruhusia kwenda nyumbani.

Tundu Lissu alipigwa risasi zaidi ya thelathini na watu ambao mpaka sasa hawajafahamika mwanzoni mwa mwezi Septembamjini Dodoma alipokuwa akihudhuria vikao vya bunge.

Ndugu zake Bw Lissu wameitaka serikali kuvishirikisha vyombo vya upelelezi vya kimataifa kama vinavyoshirikishwa katika mambo mengine ili kuongeza ufanisi katika upelelezi huo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana