Pata taarifa kuu
RWANDA-HAKI-SIASA

Mama wa Diane Rwigara akanusha mashitaka dhidi yake

Adeline Rwigara, mama wa mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Diane Rwigara amekanusha tuhma kuwa amekuwa akieneza ujumbe wa mauaji ya kimbari.

Diane Rwigara (kushoto) akabiliwa na kifungo cha miaka mingi jela kwa kutuhumiwa kuhatarisha usalama wa taifa.
Diane Rwigara (kushoto) akabiliwa na kifungo cha miaka mingi jela kwa kutuhumiwa kuhatarisha usalama wa taifa. CYRIL NDEGEYA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Aliambia Mahakama kuwa, yeye ni mwathirika wa mauaji hayo yaliyotokea mwaka 1994, na hivyo asingeweza kuhusika kusambaza ujumbe huo.

Ameshtakiwa pamoja na mwanaye na mtoto wake mwingine, Anne Rwigara na wote wamekanusha madai dhidi yao.

Mapema wiki hii Diane Rwigara alimuomba Rais Paul Kagame kumuachilia huru yeye, mamake na dadake.

Akiwa mahakamani siku ya Jumatatu, Bi Rwigara amesema kwamba serikali imefanya jaribio la kuinyamazisha familia yake pamoja na wafuasi wake tangu alipotangaza kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi uliofanyika mwezi Mei mwaka huu.

Watatu hao, ambao walikamatwa mwezi uliopita, wameshtakiwa kwa makosa ya udanganyifu na uchochezi, tuhuma ambazo wamesema zimechochewa kisiasa.

Diane Rwigara alizuiliwa kuendelea na nia yake ya kuwania nafasi ya urais wa Rwanda, uchaguzi ambao Paul Kagame alishinda kwa kishindo kwa karibu 99% ya kura zote zilizopigwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.