Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Kamishena wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Roselyn Akombe ajiuzulu

media Aliyekuwa Kamishena katika Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Roselyn Akombe https://twitter.com/search?q=Roselyn+Akombe+IEBC&ref_src=twsrc%5

Kamishena katika Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu, siku saba pekee kuelekea Uchaguzi mpya wa urais uliopangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.

Akombe ametoa tangazo hilo akiwa jijini New York nchini Marekani, na kusema kuwa hawezi kuendelea kufanya kazi katika Tume hiyo, aliyoielezea kugawanyika.

Aidha, amedokeza kuwa mazingira ya sasa ya kisiasa hayawezi kuruhusu kufanyika kwa Uchaguzi utakaokuwa huru na haki.

“Siwezi kuendelea kufanya kazi, katika mazingira kaa haya, kila dalili zinaonesha wazi kuwa Uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki,” alisema Akombe akiwa Marekani.

Bi Akombe aliondoka nchini siku ya Jumanne, kwenda Dubai kushuhudia uchapishwaji wa karatasi za kupigia kura lakini akaamua kwenda nchini Marekani, ambako pia ni raia wa nchi hiyo.

Kujiuzulu kwa Bi. Akombe, ni pigo kwa Tume hiyo ambayo ilikuwa inamtegemea kuzungumza kwa niaba yake na kuitetea mara kwa mara.

"Tume ijitokeze wazi, iwe na ujasiri na kusema kuwa Uchaguzi huu hauwezi kuwa huru na haki katika mazingira haya," aliongeza Akombe.

Amesema pia alikuwa anapata vitisho kuhusu maisha yake na huenda asirejee nchini Kenya katika siku za hivi karibuni.

Suba Churchil, kiongozi wa mashirika ya kiraia amesema hali hii inaendelea kuzua wasiwasi kuhusu Uchaguzi huo uliopangwa kufanyika wiki ijayo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana