Pata taarifa kuu
KENYA-MAANDAMANO-UCHAGUZI

Marufuku ya maandamano yaondolewa Kenya

Nchini Kenya Mahakama ya Juu imeondoa marufuku ya kuandamana dhidi ya tume ya uchaguzi ya chi hiyo IEBC. Mahakam inasema uamuzi huo ni wa muda.

Wafuasi wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance (NASA) wakitawanywa na polisi mjini Nairobi, Kenya Octobea 11, 2017.
Wafuasi wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance (NASA) wakitawanywa na polisi mjini Nairobi, Kenya Octobea 11, 2017. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Maandamano yalizuka baada ya uchaguzi wa Agosti 8, ambapo Rais Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi.

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, umeahirisha maandamano ya leo Jumanne kote nchini ili viongozi kuwatembelea wafuasi wao waliojeruhiwa na kutembelea familia zilizopoteza wapendwa wao baada ya kupigwa risasi na Polisi.

NASA imewalaumu polisi kwa kutumia nguvu nyingi dhidi ya waandamanaji, madai ambao polisi wamekana.

Wakati huo huo Mahakama ya upeo nchini Kenya imeunga mkono uamuzi wa mahakama ya rufaa unaomnyima uwezo mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kurekebisha matokeo ya uchaguzi kutoka maeneo ya bunge.

Awali Mahakama ya rufaa ilisem akuwa mwenyekiti hana uwezo wa kurekebisha matokeo bali kazi yake ni kutangaza matokeo ya uchaguzi na kuachia mahakama swala la hitilafu zilizojitokeza katika uchaguzi.

Mahakam imesema Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi anaona hitilafu , anatakiea kuelezea vyama vilivyopo, wachunguzi wa uchaguzi na raia na kuwachia swala hilo mahakama ya uchaguzi, kwa sababu si wajibu wake.

Uchaguzi mpya nchini Kenya umepangwa kufanyika Agosti 26, lakini kiongozi wa muungano wa upinzani NASA, Raila Odinga alitangaza hivi karibuni kwamba hatoshiriki uchaguzi huo mpaka pale kutakua kumefanyika mageuzi ndani ya Tume ya Uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.