Pata taarifa kuu
KENYA-MAANDAMANO-UCHAGUZI

NASA kuendelea na maandamano kabla ya siku 9 za Uchaguzi

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, unaanza maandamano ya kila siku kuanzia leo kushinikiza mabadiliko ndani ya Tume ya Uchaguzi, siku tisa kuelekea Uchaguzi mpya wa urais.

Wafuasi wa Raila Odinga wakifurahi katika mitaa ya Kibera uchaguzi mpya wa Oktoba 26, baada ya uchaguzi wa Agosti 8 kufutwa na mMahakam Kuu nchini Kenya.
Wafuasi wa Raila Odinga wakifurahi katika mitaa ya Kibera uchaguzi mpya wa Oktoba 26, baada ya uchaguzi wa Agosti 8 kufutwa na mMahakam Kuu nchini Kenya. REUTERS/ Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Licha ya maandamano haya kupigwa marufuku kaikati ya miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu, upinzani umesema utaendela na maandamano hayo.

Kiongozi wa NASA, Raila Odinga ambaye amerejea nyumbani akitokea nchini Uingereza amewaambia wafuasi wake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maandamano hayo.

Rais Uhuru Kenyatta kwa upande wake, amesema kuwa, wapinzani wanaweza kuandamana kwa amani lakini akatoa onyo iwapo watazua fujo na kupora mali ya watu.

Kumekuwepo kwa wito wa Odinga na Kenyatta kuja katika meza ya mazungumo, hasa baada ya Odinga kujiondoa kwenye uchaguzi huo, huku kukiwa na hofu kuwa huenda ngome za upinzani zishiriki katika Uchaguzi huo wa tarehe 26.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.