Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Raila Odinga: Bila mabadiliko ndani ya Tume ya Uchaguzi, hakuna Uchaguzi

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, umesisitiza kuwa hautashiriki katika Uchaguzi mpya wa urais uliopangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raïla Odinga
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raïla Odinga REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa muungano huo Raila Odinga amesisitiza hilo katika mkutano wa hadhara mjini Mombasa Pwani ya nchi hiyo baada ya kurejea nchini, akitokea nchini Uingereza siku ya Jumapili.

Odinga aliyetangaza wiki iliopita kujiondoa kwenye Uchaguzi huo, amewaambia wafuasi wake kuwa Uchaguzi huo hautafanyika kwa sababu Tume ya Uchaguzi haijafanya marekebisho kama ilivyoagizwa na Mahakama ya Juu iliyofuta matokeo ya urais mwezi Agosti.

Pamoja na hio, muungano huo umetangaza kuwa maandamano ya amani, kushinikiza mabadiliko ndani ya Tume ya Uchaguzi yataendelea wiki ijayo, kila siku kuanzia siku ya Jumatatu hadi Ijumaa.

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya ndani imepiga marufuku katikati ya miji ya Kisumu, Nairobi na Mombasa kwa kile ilichosema kuwa waandamanaji wa upinzani wanatumia maandamano hayo kupora mali ya watu.

Hata hivyo, upinzani umesema utaendelea na maandamano hayo katikati ya miji hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto wamesema licha ya maandamano na shinikizo za NASA wataendelea na maandamano, uchaguzi utaendelea.

Tume ya Uchaguzi inasema iko tayari kwa Uchaguzi huo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.