Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Maandamano mengine ya upinzani kufanyika Ijumaa nchini Kenya

media Upinzani nchini Kenya umeapa kuendelea na maandamano licha ya marufuku ya serikali. REUTERS/James Keyi

Maandamanno ya muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, yanatarajiwa nchini humo, licha kupigwa marufuku na serikali.

Siku ya Alhamisi, Waziri wa Mambo ya ndani Fred Matinag'i alisema polisi hawataruhusu maandamano kufanyika katikati ya miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu baada ya waandamanaji wiki hii kuharibu na kupora mali ya watu.

Hata hivyo, muungano wa NASA umesema maandamano hayo yatafanyika katikati ya miji hiyo. Wanaharajati wa haki za binadamu nchini humo wanasema maandamano ya amani ni haki ya raia wa nchi hiyo.

Aidha, Waziri Fred Matinag'i alibaini kwamba serikali haiwezi kuzuia maandamano kwa sababu ni haki ya wakenya kama ilivyoanishwa kikatiba, kuandamana ila inachofanya, ni kuepusha mali ya watu kuporwa na kuharibiwa.

“Tunafanya hivi ili kuzuia uharibifu wa mali ya watu na kuwalinda Wakenya wengine wasiotaka kuandamana,” alisema.

“Maandamano ni haki ya kila mtu kwa sababu hilo lipo kwenye Katiba ya nchi,” aliongeza Matiang'i.

Hata hivyo, waandalizi wa maandamano ya upinzani wakiongozwa na kiongozi wa vijana katika muungano huo Benson Musungu, wamepuuzilia mbali marufuku hayo na kusisitiza kuwa yataendelea kama ilivyopangwa siku ya Ijumaa.

Musungu amesema maandamano ya Ijumaa yataendelea kama ilivyopangwa na kila siku kuanzia Jumatatu ijayo.

Kiongozi wa muungano huo Raila Odinga ambaye ametangaza kujiondoa kwenye Uchaguzi huo kwa kile alichosema kuwa, hajaridhishwa na maandalizi ya Tume ya Uchaguzi, yupo ziarani nchini Uingereza.

Tume ya Uchaguzi inasema, uchaguzi wa tarehe 26 utaendelea kama kawaida lakini wanasheria na wachambuzi wa siasa wanaotofautiana kuhusu uhalali wa Uchaguzi huo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana