Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 13/12 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 13/12 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 12/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Ufaransa: Mmoja wa waandamanaji wanaovalia vizibao vya njao afariki baada ya kugongwa na lori Avignon
 • Raia wa pili wa Canada akamatwa nchini China
 • Uturuki: Watu wanne wapoteza maisha na 43 wajeruhiwa katika ajali ya treni Ankara (gavana)
 • Jerusalemu: Mshambuliaji avamia polisi wawili wa Israel kabla ya kuuawa (polisi)
 • DRC: Ghala la Tume ya Uchaguzi lateketea kwa moto siku kumi kabla ya uchaguzi (mamlaka)
E.A.C

Kiir: Amani iliyowekwa kwa kulazimishwa imesababisha kuzuka kwa vita

media Rais Salva Kiir amesema mataifa ya nje hayawezi kuchukua mikataba ya nchi nyingine kuiletea Sudan Kusini. REUTERS/Jok Solomun

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesisitiza kuwa, hatakubali kulazimishwa kutia saini mkataba wa amani uliondaliwa na watu kutoka nje ya nchi hiyo.

Kiir amesema mikataba iliyopita, ndio iliyosababisha machafuko zaidi nchini humo na kusema iwapo kutakuwa na mazungumzo yawe na raia wa nchi hiyo pekee.

Aidha, amesema mataifa ya nje hayawezi kuchukua mikataba ya nchi nyingine kuiletea Sudan Kusini.

Mwishoni mwa mwezi Desemba Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilikataa azimio lililoungwa mkono na Marekani la kuiwekea vikwazo vya silaha taifa la Sudan Kusini, licha ya onyo kuwa huenda taifa hilo likakumbwa na mauaji ya halaiki.

Azimio hilo lilipata kura saba kwa jumla ya kura 15 na kukosa kufikisha kura tisa ambazo zilihitajika kupitishwa azimio hilo.

Hata hivyo hivi karibuni, serikali ya Marekani iliwawekea vikwazo maofisa wawili waandamizi wa serikali ya Sudan Kusini na aliyekuwa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo kutokana na kuhusika na vita ya wenyewe kwa wenye nchini humo.

Wizara ya fedha ya Marekani ilitangaza kuwa mali zote zilizoko nchini Marekani za waziri wa habari wa Sudan Kusini Michael Makuei Leuth, makamu mkuu wa jeshi Malek Reuben na mkuu wa majeshi aliyefutwa kazi Paul Malong zimezuiliwa, na maofisa hao wamepigwa marufuku kuingia Marekani.

Serikali ya Marekani pia imeziwekea vikwazo kampuni tatu zinazomilikiwa au kudhibitiwa na mmoja wa maofisa hao.

Vikwazo hivyo vilikuja siku chache baada ya ofisa wa serikali ya Marekani kusema serikali ya Marekani inafikiria kupitia upya msaada wake kwa Sudan Kusini.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana