Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Kenyata kutia saini muswada tata kuwa sheria

media Rais Uhuru Kenyatta akikutana na wafuasi wake katika eneo la Burma Market ,Sptemba 1, 2017. REUTERS/Thomas Mukoya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kutia saini, mswada tata kuwa sheria baada ya bunge la taifa na Senate kuyafanyia marekebisho sheria za Uchaguzi.

Wabunge na Maseneta wa upinzani walisusia vikao vyote vya kufanya mabadiliko hayo, kwa kile walichosema kuwa mabadiliko hayo yalikuwa kwa nia mbaya na yalikuwa yanampendelea rais Kenyatta kuelekea Uchaguzi mpya.

Wakati huo huo, kiongozi wa muungano NASA Raila Odinga ambaye ametangaza kujitoa kwenye kinyang'ayiro cha urais nchini humo, anaendela na ziara yake nchini Uingereza ambako amekuwa akikutana na viongozi mbalimbali kuwaelezea hali ya kisiasa nchini Kenya.

Hayo yanajiri wakati ambapo upinzani nchini humo umeapa kuendelea na maandamano Ijumaa hii kushinikiza kufanyika mageuzi kwenye tume ya uchaguzi IEBC licha ya serikali kupiga marufuku maandamano yyoyote katikati ya miji mikuu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana