Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA

Chama cha FDC chazindua kampeni ya kupinga mageuzi ya Katiba Uganda

Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Ugandacha FDC wamezindua kampeni ya kupinga kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo.

Chama cha FDC cha Kizza Besigye( kwenye Picha) kimezindua kampeni dhidi ya mageuzi ya Katiba.
Chama cha FDC cha Kizza Besigye( kwenye Picha) kimezindua kampeni dhidi ya mageuzi ya Katiba. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya chama tawala cha NRM kuwasilisha mswada bungeni kutaka katiba kubadilishwa na kuondolewa kwa kikomo cha umri kwa yeyote anayetaka kuwania urais nchini humo kutoka miaka 75.

Aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha upinzani cha FDC, Kizza Besigye, amekuwa katika mstari wa mbele kupinga mabadiliko hayo lakini pia kutoa wito kwa watu kuacha magari yao na kupanda mabasi ya umma kwenda kazini kila siku ya Jumanne.

Mgogoro wa kisiasa nchi Uganda unaendelea, huku wananchi wengi wa nchi hiyo wakiwa na hofu ya kuzuka kwa vurugu.

Muswada wa Marekebisho ya katiba ulizua ghasia wakati wa kuwasilishwa Bungeni ambapo mvutano mkubwa baina ya wabunge wa upinzani na wale wa chama tawala ulishuhidwa huku wabunge hao wakirushiana makonde.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.