Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Wagombea walioshiriki uchaguzi wa kwanza ruksa kushiriki uchaguzi ujao Kenya

media Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC), Wafula Chebukati. REUTERS/Baz Ratner

Uchaguzi wa rais nchini Kenya utafanyika kwa tarehe iliyopangwa ya Oktoba 26. Tume ya Uchaguzi ilitangaza siku ya Jumatano jioni kwa taarifa yake, kufuatia mkutano uliandaliwa kwa minajili ya kutoa mwanga kuhusu suala hili.

Tangazo hilo linakuja siku moja baada ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kutangaza kujiondoa katika uchaguzi wa Oktoba 26.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC, uchaguzi huo utajumuisha wagombea wanane ambao walishiriki uchaguzi wa kwanza wa tarehe 8 Agosti. Uchaguzi ambao ulifutwa na Mahakama Kuu ya Kenya kwa sababu ya makosa yaliyogubika uchaguzi huo.

Wagombea sita ambao hawakufanikiwa kupata kura zinazohitajika ambao walikua wakidai kushiriki katika uchaguzi wa Oktoba 26 wamepewa nafas ya kushiriki.

Raila Odinga pia amealikwa kushiriki katika uchaguzi huo. Hii inamaanisha kuwa tume ya uchaguzi hainazingatii uamuzi wake wa kujiondoa, ikibaini kwamba kiongozi huyo wa upinzani hakutoa maaelezo sahihi. Raila Odinga hata hivyo, alielezea kuwa hatashiriki uchaguzi wa Oktoba 26 kama hakutakua na mageuzi kamili ya tume ya uchaguzi. Bw. Odinga anashtumu Tume ya Uchaguzi IEBC kuficha makosa ambayo yaliharibu uchaguzi wa kwanza.

Wagombea wengi wanaunga mkono madai ya muungano wa upinzani. Kwa upande wa mwanasheria wa Ekuru Aukot, kiongozi wa muungano wa tatu wa Kenya, ambaye alichukua nafasi ya tatu katika uchaguzi wa mwezi Agosti, anasema mabadiliko yanahitajika kufanywa ndani ya tume ya Uchaguzi.

Tume ya Uchaguzi inasema katika taarifa yake kuwa haiwezi kumlazimisha mgombea kushiriki tena ikiwa atakataa.

IEBC imetoa wit kwa utulivu na mazungumzo.Uchaguzi lazima ufanyike na nchi iendelee kusonga mbele, Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC imesema katika taarifa yake.

Wakati huo huo uhamasishaji wa upinzani unaendelea. "Hakuna marekebisho, hakuna uchaguzi", haya ni maeneo yaliyokua yakitolewa wakati wa maandamano yaliyofanyika Kisumu katika maeneo yanayoonekana kama ngome za upinzani.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana