Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Serikali ya Kenya yapiga marufuku maandamano ya upinzani katikati ya miji

media Maandamano ya upinzani nchini Kenya, yaliyofanyika jijini Nairobi Oktoba 11 2017 REUTERS/Thomas Mukoya

Serikali ya Kenya imetangaza kupiga marufuku maandamano ya wafuasi wa upinzani NASA  katikati ya miji  nchini humo.

Waziri wa Usalama na Mambo ya ndani  Fred Matiang'i, amesema maandamano hayo hayataruhusiwa katikati  ya jiji la Nairobi, Mombasa na Kisumu.

Matiang'i ameongeza  kuwa hatua hii imechukuliwa baada ya baadhi ya waandamanaji wa upinzani kupora mali ya watu katika miji hiyo siku ya Jumatano.

Aidha, Waziri huyo amefafanua kuwa serikali haiwezi kuzuia maandamano kwa sababu ni haki ya wakenya kama ilivyoanishwa kikatiba, kuandamana  ila inachofanya, ni kuepusha mali ya watu kuporwa na kuharibiwa.

“Tunafanya hivi ili kuzuia uharibifu wa mali ya watu na kuwalinda Wakenya wengine wasiotaka kuandamana,” alisema.

“Maandamano ni haki ya kila mtu kwa sababu hilo lipo kwenye Katiba ya nchi,” aliongeza Matiang'i.

Hata hivyo, waandalizi wa maandamano ya upinzani wakiongozwa na kiongozi wa vijana katika muungano huo Benson Musungu, wamepuuzilia mbali marufuku hayo na kusisitiza kuwa yataendelea kama ilivyopangwa siku ya Ijumaa.

Musungu amesema maandamano ya Ijumaa yataendelea kama ilivyopangwa na kila siku kuanzia Jumatatu ijayo.

Kiongozi wa muungano huo Raila Odinga ambaye ametangaza kujiondoa kwenye Uchaguzi huo kwa kile alichosema kuwa, hajaridhishwa na maandalizi ya Tume ya Uchaguzi, yupo ziarani nchini Uingereza.

Tume ya Uchaguzi inasema, uchaguzi wa tarehe 26 utaendelea kama kawaida lakini wanasheria na wachambuzi wa siasa wanaotofautiana kuhusu uhalali wa Uchaguzi huo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana