Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Balozi Berak: Adhabu ya kifo haina nafasi katika dunia ya sasa

media Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak akifanya mahojiano na mwandishi wa rfikiswahili (hayuko pichani). April 6, 2017, RFI

Serikali ya Ufaransa imesema itaendelea kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa kuhamasisha mataifa ya Afrika kuondoa adhabu ya kifo katika nchi zao.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Malika Berak amesema serikali za Afrika, wadau wa haki za binadamu na asasi za kiraia zina jukumu kubwa katika kufanikisha hatua hiyo.

Malika Berak - Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania kuhusu adhabu ya kifo 12/10/2017 Kusikiliza

“Hili ni jukumu la ulimwengu mzima, Tanzania imeonyesha njia kwa kutotekeleza adhabu ya kifo tangu mwaka 1994”.

Balozi Berak amesema serikali ya Ufaransa itaendelea kutimiza wajibu wake kwa kutumia maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuondoa adhabu ya kifo kuandaa mijadala itakayowakutanisha wadau kutoka serikalini, asasi za kiraia na jamii kwa ujumla ili kukuza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kuondoa adhabu hiyo.

John Nyoka - Afisa Magereza wa zamani kwa nchi za Tanzania na Namibia 12/10/2017 Kusikiliza

Kwa upande wake kamishna wa zamani wa magereza katika nchi za Tanzania na Namibia, John Nyoka amesema mataifa mengi ya Afrika yamekuwa yakisita kuondoa adhabu ya kifo kutokana na kuongezeka kwa makosa ya jinai.

Raia wa Uganda Susan Kigula ambaye alihukumiwa adhabu ya kifo nchini Uganda kabla ya kuachiliwa huru alisema adhabu ya kifo si suluhu ya kukomesha uhalifu duniani.

“Hili ni suala la uelewa, nilitumia uzoefu na elimu yangu kupinga adhabu ya kifo katika mahakama ya Uganda na mahakama iliondoa adhabu ya kifo,”

Kongamano la kujadili siku ya kimataifa ya kuondoa adhabu ya kifo liliandaliwa na ubalozi wa Ufaransa na kufanyika Jijini Dar es Salaam Oktoba 10.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana