Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Polisi yazima maandamano ya upinzani nchini Kenya

media  
Maandamano ya muungano wa upinzani NASA, Kisumu, Oktoba 6, 2017. REUTERS/James Keyi

Siku moja baada ya kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga kutangaza kujiondoa katika kinyang'anyiro cha urais kiliyopangwa kufanyika Oktoba 26, wafuasi wa upinzani wamemiminika Jumatano hii katika mitaa ya miji mbalimbali nchini humo.

Waandamanji wanadai maafisa wa Tume ya uchaguzi IEBC wajiuzulu na kuteuliwe wengine wakiwashtumu kula njama na chama tawala cha Jubilee katika uchaguzi wa urais ulifutwa na Mahakama ya Juu nchini Kenya

Polisi nchini Kenya wamerusha mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa muungano wa upinzani ambao wamekuwa wakiandamana mjini Kisumu, magharibi mwa nchi hiyo.

Maandamano pia yamefanyika katika miji mingine mikuu ingawa hali imekuwa tulivu.

idadi ya waliojitokeza walikuwa wengi kuliko maandamano ya awali..

Muungano wa Nasa umekuwa ukifanya maandamano kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa kushinikiza mageuzi katika Tume ya uchaguzi (IEBC) kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mpya.

Wakati huo huo Mahakama Kuu imeagiza kushirikishwa kwa mgombea wa Thirdway Alliance Dkt Ekuru Aukot kwenye uchaguzi huo.

Hata hivyo Muungano wa upinzani Nasa unataka uchaguzi mpya ufanyike katika kipindi cha siku zisizozidi 90 na wagombea wateuliwe upya.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana