Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Watu waliojihami kwa silaha wawapiga risasi na kuwauwa watu wawili Pwani ya Kenya

media Maafisa wa Polisi mjini Mombasa wakiweka ulinzi katika siku zilizopita, katika harakati za kupambana na ugaidi reutersmedia.net

Wafanyikazi wawili wa Chuo Kikuu cha Mombasa, tawi la Kwale Pwani ya Kenya wamepigwa risasi na kuawa na watu wasiojulikana waliokuwa wamejihami kwa silaha.

Maafisa wawili wa Polisi na dereva wa gari walimokuwa wanasafiria wamejeruhiwa katika tukio hilo lilitokea siku ya Jumanne asubuhi.

Maafisa wa Polisi walikuwa wanawasindikiza wafanyikazi hao wa Chuo Kikuu waliposhambuliwa kwa kushtukiza.

Kamanda wa Polisi katika Kaunti ya Kwale, Larry Kieng amethibitisha kutokea kwa tukio hili.

Aidha, ameeleza kuwa wafanyikazi hao wawili waliuawa papo hapo, lakini waliojeruhiwa wanaendelea kupata matibabu hospitalini mjini Kwale.

Pamoja na hilo, ameongeza kuwa uchunguzi unaendelea lakini anashuku wanamgambo wa Al Shabab kutoka Somalia ndio waliohusika.

Miezi miwili iliyopita, washukiwa wa Al Shabab walivamia Kanisa moja katika eneo hilo la Kwale na kuwauwa polisi wawili waliokuwa wanatoa ulinzi na kuiba bastola zao.

Kwale na maeneo kadhaa ya Pwani ya Kenya kama Lamu yameendelea kulengwa na kundi la kigaidi la Al Shabab.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana