Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

MSF Tanzania yasema magonjwa ya akili yameongezeka katika kambi ya wakimbizi ya Nduta

media Kambi ya wakimbizi ya Nduta nchini Tanzania, inayowapa hifadhi wakimbizi kutoka Burundi MSF

Shirika la Kimataifa la Madktari wasiokuwa na mipaka, Médecins Sans Frontières (MSF), linasema kuna ongezeko mkubwa wa kiwango cha magonjwa ya akili katika kambi ya wakimbizi ya Nduta katika jimbo la Kigoma nchini Tanzania.

Utafiti wa MSF unaonesha kuwa kati ya wakimbizi 127,000 wanaotoka nchini Burundi wanaoishi katika kambi hiyo, kila mwezi kuna watu 400 wanaotafuta ushauri na matibabu ya akili ili kupata msaada.

Ripoti ya MSF inaeleza kuwa, robo tatu ya wagonjwa wa akili katika kambi hiyo ni wanawake.

Hali ya Msongo wa mawazo imeelezwa kuwa sababu kubwa inayosababisha magonjwa hayo ambayo imeelezwa ni kwa asilimia 30.1.

Wale wanaopata tatizo hili kutokana na wasiwasi na mashaka, ni asilimia 28.5 huku maumivu ya kimwili ikiwa ni kwa asilimia 11.0.

MSF inasema sababu kubwa ya ongezeko hili, ni maisha magumu ya wakimbizi kambini.

“Tunaamini kuwa, matatizo mengi ambayo wakimbizi wanapitia katika kambi ya Nduta, ndio chanzo cha ongezeko la watu kwenda kutafuta msaada wa matibabu,” amesema Kristi Payten, Mkuu wa maswala ya matibabu kutoka Shirika la MSF nchini Tanzania.

MSF imekuwa katika mstari wa mbele kutoa huduma za matibabu katika kabi ya Nduta kuanzia mwezi Mei mwaka 2015.

Shirika hilo linasema limetoa msaada wa kisaikolojia kwa watu 40,070 kwa watu binafsi na familia katika kambi hiyo ya wakimbizi.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana