Pata taarifa kuu
RWANDA-HRW-HAKI

Human Right Watch yaishtumu Rwanda kuwatesa mahabusu

Shirika la kimataifa la haki za Binadamu la Human Right Wacht limetoa linaishtumu serikali ya Rwanda kuwatesa wafungwa katika jela mbalimbali za kijeshi nchini humo.

Kigali, mji mkuu wa Rwanda.
Kigali, mji mkuu wa Rwanda. Getty/Peter Stuckings
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti ya leo, shirika la Human Right Watch limesema watu wanaoshtumiwa kushirikiana na kundi la waasi la FDLR na RCN wamekua wakiteswa kwa kuwekewa vitu vizito kwenye nyeti zao au kuadhibiwa kwa kwa shoti za umeme katika kambi za kijeshi nchini humo.

Hata hivyo serikali ya Rwanda imekanusha shutma hizo dhidi yake.

Miezi mitatu iliyopita Human Right Watch lilibaini kwamba vikosi vya usalama nchini Rwanda viliwaua takriban watu 37 wanaoshukiwa kufanya makosa madogo madogo tangu mwezi Aprili 2016.

Ripoti hiyo ilisema kuwa hatua hiyo inaonekana kuwa mpango wa makusudi kuwaua washukiwa wa wizi.

HRW ilisema mwaka 2015 kwamba ilikuwa imenakili kukamatwa maelfu ya watu wakiwemo watoto wa kurandaranda mitaani pamoja na makahaba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.