Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Ripoti: Watu 37 walipoteza maisha nchini Kenya baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti

media Makabiliano kati ya waandamanaji na polisi mtaani Mathare jijini Nairobi www.reuters.com

Watu 37 walipoteza maisha baada ya kuzuka kwa machafuko ya baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya mwezi Agosti mwaka huu.

Takwimu hizi zimetolewa katika ripoti ya Tume ya taifa ya kutetea haki za Binadamu.

Tume hiyo imesema takwimu hizo zimekusanywa kipindi chote wakati machafuko hayo yalitokea kati ya tarehe 9 na 15 mwezi Agosti katika ngome za upinzani Magharibi mwa nchi hiyo na jijini Nairobi.

Imebainika kuwa, watu waliopoteza maisha walikabiliana na polisi wa kupambana na ghasia na kusababisha watu wengine 126 kujeruhiwa.

Maeneo yaliyoathiriwa wakati wa machafuko hayo ni mitaa iliyo na wafuasi wa upinzani jijini Nairobi ikiwemo Kawangware, Mathare, Kibra, Lucky Summer, Baba Dogo na Huruma.

Watu wengine waliuawa na kujeruhiwa katika makabiliano kama hayo mjini Kisumu katika mitaa ya Kondele, Manyatta, Nyamasaria na Nyalenda.

Ngome nyingine za upinzani mjini Siaya, Ugunja, Rangwe na Homa Bay, Magharibi mwa nchi hiyo pia ziliathirika.

Mtoto wa miezi sita Samantha Pendo, ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha katika vurugu zilizozuka baada ya Tume ya Uchaguzi kumtangaza Uhuru Kenyatta kama mshindi wa Uchaguzi wa urais nchini humo.

Ripoti hiyo ya zaidi ya kura 600, imeeleza kuwa watu walipoteza maisha walikuwa ni kati ya miaka 20 na 45.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana