Pata taarifa kuu
RWANDA-HAKI-SIASA

Diane Rwigara afikishwa mahakamani

Mwanaharakati aliyejaribu kuwania kiti cha urais nchini Ijumaa hii kujibu mashtaka ya kuchochea uasi nchini mwake.

Diane Rwigara akabiliwa na kifungo cha miaka mingi jela kwa kutuhumiwa kuhatarisha usalama wa taifa..
Diane Rwigara akabiliwa na kifungo cha miaka mingi jela kwa kutuhumiwa kuhatarisha usalama wa taifa.. CYRIL NDEGEYA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ilikuwa yapata mida wa saa nne asubuhi kwa saa za Afrika ya kati, ndipo mwanadada huyo ambaye alikuwa ameongozana na mama yake pamoja na mdogo wake, wamefikishwa katika mahakama ya Nyarugenge wakiwa wamevaa pingu mikononi huku mama yake akiwa ameshika bibilia na wakati akiondoka amepepea watu wa familia yake kama ishara kwamba bibilia ndiyo ngao yake.

Mara baada ya kuwasili wameingia ndani ya chumba cha mahakama na kuomba kesi yao iahirishwe kwani hawakuwa na mawakili.

Wamedai kwamba, mmoja kati yao hakuwa na wakili na wawili ambao ni mwanasiasa Diana Rwigara na mama yake ndiyo waliokuwa na wakili lakini hawakupata muda wa kuzungumza naye na hakuwepo mahakamani hapo.

kwa kuzingatia sheria kwamba mtuhumiwa ana haki ya kuwa na wakili pindi atakapo iwe hivyo, kesi imelazimika kuahirishwa hadi tarehe tisa mwezi oktoba mwaka huu yaani jumatatu ijayo.

Ikumbukwe Diana Rwigara alitangaza nia ya kugombea kiti cha urais kama mgombea huru mwezi Juni mwaka huu lakini hakufanikiwa kutokana na kile ambacho tume ya taifa ya uchaguzi nchini humu NEC, ilidai kwamba hakuwa na vigezo vya kutosha.

Anatuhumiwa kwa makosa ya kuchochea uasi pamoja na kugushi nyaraka mama huku mama yake akituhumiwa kwa kosa la kuchochea ukabila na mdogo wake aitwaye Ana Rwigara anatuhumiwa kwa kosa la kuzua vurugu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.