Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Wabunge wa upinzani waendelea kupata vitisho nchini Uganda

media Wabunge wa upinzani nchini Uganda wanasema kuwa wameanza kulengwa na mashambulizi ya gruneti na vitiso vingine. REUTERS/James Akena

Nchini Uganda, sula ambalo limekua gumzo ni lile la marekebisho ya Katiba kuhusu ukomo wa umri wa rais Museveni kuendelea kuwania kiti cha urais nchini humo.

Rasimu ya marekebisho ya Katiba itamruhusu Museveni ambaye yuko madarakani kwa zaidi ya 30 miaka, kuwania muhula mwingine mnamo mwaka 2021.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI mjini Kampala, Charlotte Cosset, wabunge wa upinzani wanaendelea kukabiliwa na vitisho na hata mashambulizi ya kimwili. Siku ya Jumanne, rasimu ya ya marekebisho ya Katiba iliwasilishwa bungeni kwa ajili ya kusomwa kwa kwanza. Hata hivyo wabunge wachache wa upinzani ndio walikua walishiriki kikiao hicho,

Nakala iliwasilishwa rasmi bungeni kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya kwanza. Lakini licha ya idadi kubwa ya wabunge wa chama tawala na washirika wake, viti vya wabunge wa upinzani vilisali tupu. Edson Kafuuzi, mmoja wa wanaharakati wa marekebisho ya Katiba amesema upinzani haipaswi kubeba lawama.

"Wao hawako hapa kwa sababu wamesimamishwa au wamechukua uamuzi wa kujitenga nasi. Kwa hiyo hali hii haina uhusiano na vitisho. Hata kwa sisi wasaidizi wa muswada huu tunapokea vitisho. Tatizo pekee ambalo ninaona ni kwamba wenzetu katika upinzani walianza kile walichokiita upinzani kama fomu ya maandamano lakini ni kuchochea vurugu. »

Katika muda wa wiki moja, gruneti zilirushwa mbele ya makazi ya wabunge watatu wa upinzani. Jumanne asubuhi nyumbani kwa Bobi Wine, mwimbaji maarufu ambaye hivi karibuni aliingia katika siasa alikumbwa na hasara kubwa baada ya kushambuliwa kwa gruneti .

Mwimbaji huyo maarufu amesema hashangazwi na mashambulizi haya.

«Kabla ya hapo nimekuwa nikipokea ujumbe usiojulikana unanionya mimi kuacha kupinga kuondolewa kwa kikomo cha umri au nitauawa. Haya yote yamekusudiwa kwa maoni yangu kwa kunitisha na familia yangu. Lakini ninawaambia watu hao kwamba sijalitishio siogopi kubadili nia yangu ya kulinda Katiba. »

Kamati ya kisheria sasa ina siku 45 ili kuwasilisha upya nakala hii bungeni kwa minajili ya kujadiliwa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana