Pata taarifa kuu
BURUNDI-UN-HAKI-USALAMA

Umoja wa Mataifa waendelea na uchunguzi wake kuhusu Burundi

Tume ya haki za Binadamu ya Umoja wa mataifa imepitisha azimio mpya kuhusu nchi ya Burundi baada ya uchunguzi uliobaini kuwa mauaji, utesaji na ukamataji wa raia umekuwa ukiendelea.

Mwandishi wa Burundi Jean Bigirimana aliyepotea zaidi ya mwaka uliopita, Julai 22, 2016, karibu na mji wa Bujumbura. Idara ya ujasusi Burundi inanyooshewa kidole.
Mwandishi wa Burundi Jean Bigirimana aliyepotea zaidi ya mwaka uliopita, Julai 22, 2016, karibu na mji wa Bujumbura. Idara ya ujasusi Burundi inanyooshewa kidole. STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Azimio hilo liliwasilishwa dakika za mwisho mbele ya tume hiyo ya umoja wa mataifa inayoshughulikia masuala ya haki za binadamu na kundi la wataalamu kutoka bara la Afrika, ambao walitembelea mji mkuu wa Burundi, Bujumbura ambako walikusanya ripoti nyingi kuhusu kupotea kwa watu, mauaji ya kuvizia na ukiukwaji mkubwa wa Haki za binadamu nchini humo.

Azimio hili limependekeza kutumwa kwa timu mpya ya wataalamu watatu wa umoja wa mataifa wa haki za binadamu ambao watashirikiana na wakuu wa serikali ya Bujumbura kuchunguza visa vya uhalifu dhidi ya binadamu, mauaji, unyanyasaji unaodaiwa kufanyika nchini humo.

Wachambuzi wa siasa wanasema azimio hili jipya ni jibu kwa maombi ya serikali ambayo tangu mwanzoni ilitupilia mbali ripoti ya mwanzo ya tume hiyo ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa ikisema kuwa haikushirikishwa katika uchunguzi wa awali.

Kumekuwa na hali ya vuta ni kuvute kati ya serikali ya Bujumbura na tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu kuhusu ripoti iliyotolewa mwezi mmoja uliopita ikibainisha kuendelea kwa vitendo vya mauaji, udhalilishaji, na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Burundi.

Wakati huo huo shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu la Amnesty International limeonya kuwa Maelfu ya wakimbizi wa Burundi wanaorudi nchini kwao kutoka Tanzania wanakabiliwa na hatari za kiusalama nchini mwao.

Mwezi uliopita, Tanzania, Burundi na shirika la umoja wa mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR walikubaliana kwamba kufikia mwisho wa mwaka huu wawe wamewarejesha wakimbizi elfu kumi na mbili wanaoishi Tanzania na wanataka kurudi kwao Burundi kwa hiari.

Lakini Amnesty International linasema, mpango huu unahatarisha maisha ya maelfu ya wakimbizi na linaamini kuwa wakimbizi wengi wanarejeshwa nyumbani kwao kutokana msukumo wa ushawishi kutoka serikali ya Tanzania na Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.