Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

IEBC kukutana na vyama vya Jubilee na NASA kabla ya uchaguzi

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC imepanga kukutana na wawakilishi wa chama tawala Jubilee na wale wa upinzani NASA, kuelekea Uchaguzi wa urais mwezi ujao.

Maafisa wa kupambana na ghasia nchini Kenya, GSU wakiwa mbele ya majengo ya Tume ya Uchaguzi nchini Kenya jijini Nairobi
Maafisa wa kupambana na ghasia nchini Kenya, GSU wakiwa mbele ya majengo ya Tume ya Uchaguzi nchini Kenya jijini Nairobi James Shimanyula/ RFI Kiswahili Correspodent in Nairobi
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kutoa mwaliko huo, haijafahamika vema iwapo mkutano huo utafanyika baada ya pande zote mbili katika siku zilizopita kuonekana kuwa na misimamo ya kutotaka kushauriana na tume hiyo.

Muungano wa upinzani NASA, ulioanza maandamano siku ya Jumanne wiki hii kushinikiza mabadiliko ndani ya tume hiyo, unasema uchaguzi huo hauwezi kufanyika iwapo masharti yao hayatashughulikiwa.

Naye rais Uhuru Kenyatta atakayepambana na Odinga katika uchaguzi huo mpya, amesema mpinzani wake hana mamlaka ya kushinikiza mabadiliko hayo.

Umoja wa Mataifa kupitia Shirika linalohusika na maswala ya mipango na maendeleo, UNDP, linsema liko tayari kusaidia katika maandalizi ya uchaguzi huo lakini pande mbili za kisiasa nchini humo hazitaki usaidizi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.