Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Bunge kukutana tena Jumatano hii nchini Uganda

media Kikao cha bunge kiliahirishwa baada ya wabunge wa upinzani kuvuruga shughuli za bunge na kuzuia wabunge wa chama tawala cha NRM kushindwa kuwasilisha mswada wa kuibadlisha Katiba. REUTERS/James Akena

Wabunge nchini Uganda wanatarajiwa kurejea bungeni leo saa nane mchana kujadili na kupitisha au la mswada wa kuibadlisha Katiba.

Kikao cha jana kiliahirishwa baada ya wabunge wa upinzani kuvuruga shughuli za bunge hilo na kuzuia wabunge wa chama tawala cha NRM kushindwa kuwasilisha mswada wa kuibadlisha Katiba.

Wabunge wa NRM wanataka Katiba kubadalishwa ili kifungu kinachomzuia mtu kuwania urais akiwa na zaidi ya miaka 75 kuondolewa.

Hata hivyo, wabunge wa upinzani ambao jana walivuruga shughuli za bunge kwa kuimba wimbo wa taifa wakiwa wamejifunga vitambaa vyekundu, wameapa kutoruhusu mabadiliko hayo.

Wabunge wa upinzani nchini Uganda kwa mara nyingine tena jana walifanikiwa kuzuia wabunge wa chama tawala wasilisha ombi la kutaka kuandaliwa kwa mswada wa kubadilisha Katiba ya nchi hiyo ili kuondoa kifungu kinachozuia mtu yoyote kuwania urais akiwa zaidi ya miaka 75.

Mwaka 2012 wakati akihojiwa na kituo cha NTV Uganda, rais Museveni alinukuliwa akisema haamini kuwa kiongozi anaweza kuwa na uwezo wa kufanya kazi vema akiwa na zaidi ya miaka 75.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana