Pata taarifa kuu
RWANDA-UCHAGUZI-SIASA

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Rwanda akamatwa

Mwanaharakati aliyejaribu kuwania kiti cha urais nchini Rwanda, Diane Rwigara, mama yake pamoja na dada yake, wameendelea kushikiliwa na polisi jijini Kigali. Mama wa mwanasiasa huyo pamoja na dadake wanatuhumiwa kukwepa kulipa kodi.

Kiongozi mkuu nchini Rwanda Diane Rwigara katika jengo la Tume ya Uchaguzi, Juni 20, 2017.
Kiongozi mkuu nchini Rwanda Diane Rwigara katika jengo la Tume ya Uchaguzi, Juni 20, 2017. REUTERS/Jean Bizimana
Matangazo ya kibiashara

Wakati huu ni rasmi, Mwanasiasa huyo wa upinzani Diane Rwigara, dada yake na mama yao wamekuwa wakishikiliwa tangu mwishoni mwa juma lililopita ambapo kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na msemaji wa polisi wa Rwanda, Theos Badege, ni kuwa kando na makosa ya ulaghai na kukwepa kulipa kodi, watatu hao walikuwa ni tishio kwa usalama wa nchi na wanazuia uchunguzi.

Badege amesema watatu hao wamekamatwa kufwatia uamuzi wa maafisa wakuu wa polisi kwa sababu ya kushindwa kuripoti katika idara ya upelelezi ya polisi CID kwa mara kadhaa, huku wakitapanya habari zinazo hatarisha usalama wa taifa hilo.

Kabla ya kukamatwa kwa watatu hao, polisi walifanya msako kwenye makazi anamoishi mwanasiasa huyo na familia yake mtaa wa Kiyovu mjini Kigali na kuruka juu ya lango baada ya kukataliwa kufunguliwa na kumkamata mwanasiasa huyo Mamake pamoja na dadake.

Diane Rwigara anashutumia kwa kosa la kutumia vyeti vya kughushi wakati akiwania kiti cha urais katika uchaguzi wa agosti nne mwaka huu, wakati Mama wa mwanasiasa huyo pamoja na dadake wanatuhumiwa kukwepa kulipa kodi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.