Pata taarifa kuu
RWANDA-HAKI

Kesi ya makada wa chama cha FDU yafunguliwa nchini Rwanda

Kesi ya wanachama wa chama cha upinzani nchini Rwanda cha UDF ilifunguliwa siku ya Alhamisi Septemba 21. makada hao wa chama cha FDU wanakabiliwa na shutma za kujaribu kuanzisha kundi la waasi.

Mji mkuu wa Rwanda, Kigali.
Mji mkuu wa Rwanda, Kigali. Getty/Peter Stuckings
Matangazo ya kibiashara

Boniface Twagirimana, naibu kiongozi wa chama cha FDU (Unified Democratic Forces) alifikishwa jana mahakamani kwa mara ya kwan. Chama cha Victoire Ingabire, kiongozi wa upinzani anayezuiliwa jela tangu mwaka 2011, anawatambua watu 7 kati ya wanane kama wanachama wa chama chake ambao wote walikua wameriboti mahakaman. Wote wanashtakiwa kwa kujaribu kuanzisha kundi la waasi.

Chama cha FDU kimefutilia mbali tuhuma hizo na kudai kuwa ni uzushi mtupu. Kesi ya jana haikusikilizwa kwa undani zaidi, ilikua tu swala la uwezekano wa kuachiwa huru kwa dhamana. Uamuzi uliahirishwa hadi leo, Ijumaa, Septemba 22.

Chama cha UDF pia kina wasiwasi juu ya mwanachama wake mwingine ambaye hakuwepo wakati kesi hiyo ikifunguliwa. Theophile Ntirutwa alikamatwa tarehe 6 Septemba katika operesheni kabambe ya polisi dhidi ya wafuasi na makada wa chama cha FDU. Lakini polisi ilikua ilikanusha kukamatwa kwa Bw Ntirutwa. Joseph Bukeye, Naibu kiongozi wa FDU, alikuwa na matumaini ya kumwona tena upande wa washtumiwa. Ana hofu kuwa huenda aliuawa wakati alipokua kizuizini.

"Ni ajabu sana kwa sababu hakuwa peke yake alipokamatwa. Alikamatwa kwa wakati mmoja na mwanachama mwingine wa upinzani. Na polisi hawawezi kukataa kwa sababu alikamatwa na kuwekwa ndani ya gari ya polisi na tuna namba za usajili za gari ambayo ilimbeba. Kwa hiyo tunajiuliza kwa nini hakuweza kuonekana. Polisi inajua hali hiyo" amesem aBw Bukeye.

Serikali nchini Rwanda imekua ikinyooshewa kidole cha lawama kwa kuminya wanasiasa wa upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.