Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

IEBC:Uchaguzi mpya kufanyika tarehe 26 Oktoba Kenya

Siku moja baada ya Mahakama Kuu nchini Kenya kutoa uamuzi wake wa mwisho uliofuta uchaguzi wa urais nchini humo, Tume ya uchaguzi IEBC imetangaza tarehe 26 mwezi Otoba 2017 kama tarehe mpya ya uchaguzi wa marudio.

Sanduku za kura katika kituo cha kuhesabu kura mjini Mombasa, Kenya, tarehe 9 Agosti 2017 (picha ya zamani).
Sanduku za kura katika kituo cha kuhesabu kura mjini Mombasa, Kenya, tarehe 9 Agosti 2017 (picha ya zamani). © REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Tarehe hiyo imetangazwa ikiwa ni siku tano tu kabla ya kukamilika kwa siku 60 zilizowekwa kikatiba kufanyika kwa uchaguzi mpya.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo IEBC Wafula Chebukati ametangaza kuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kuhakikisha kuwa tume tume anayoongoza imejiandaa vilivyo.

.“IEBC inaendelea kuangazia uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu kwa lengo la kutaka kuelewa madhara yake kuhusu uchaguzi mpya, “amesemaWafula Chebukati katika taarifa fupi.

Rais anayemaliza muda wake Huru Kenyatta alikua aliibuka mshindi wa uchaguzi wa urais ambao matokeo yake yalifutwa na mMahakama Kuu nchini Kenya.

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) inahidi kutoa maelezo zaidi leo Ijumaa Septemba 22. Serikali, kwa upande wake, imetoa dola milioni 97 kwa ajili ya uchaguzi huu mpya, ambao iutajadiliwa bungeni siku ya Jumanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.