Pata taarifa kuu
ZANZIBAR-USHOGA-HAKI

Watu 20 wakamatwa kwa kushtumiwa ushoga Zanzibar

Nchini Tanzania, watu 20 wanaotuhumiwa ushoga walikamatwa katika kisiwa cha Zanzibar na polisi walipokuwa wakati ambapo walikua wakishiriki semina kuhusu UKIMWI iliyoandaliwa na shirika moja lilsilo la kiserikali, vyanzo vya habari vimearifu.

Stone Town.moja ya miji ya Zanzibar.
Stone Town.moja ya miji ya Zanzibar. RFI
Matangazo ya kibiashara

Watu ishirini wanaotuhumiwa ushoga, ikiwa ni pamoja na wanawake kumi na mbili, walikamatwa Zanzibar, ilisema Jumamosi polisi ya Zanzibar.

"Watu hawa wanahusika katika shughuli za ushoga. Tuliwakamata na tuko katika mchakato wa kuwahoji. Polisi hawezi kufumbia macho kitendo hiki, "Mkuu wa polisi Zanziba Hassan Ali Nasri alisema Jumamosi kwenye televisheni ya serikali ya Tanzania TBC1. Afisa huyu wa polisi hakueleza tarehe ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao, lakini alisema kuwa wanawake kumi na wawili na wanaume wanane walihusika.

Kwa mujibu wa televisheni ya taifa, watu hao walikamatwa katika hoteli moja ambapo walikua wakipewa mafunzo na shirika lisilo la kiserikali la International Bridge Initiative NGO, ambalo limesajiliwa rasmi na serikali ya Zanzibar kwa kutoa programu za elimu kwa mapambano dhidi ya Ukimwi.

Ushoga wa kiume hupigwa marufuku nchini Tanzania na wakati mwingine unaweza kusababisha kifungo cha maisha jela. Na kama, hadi wakati huo, kulikuwa na uvumilivu, tangu mwaka mmojauliyopita mamlaka azimio kali dhidi ya ushoga.

Mapema mwaka huu, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitishia kutoa orodha ya viongozi na wasanii wanaoshukiwa kujihusisha na kitendo cha ushoga.

Wakati huo huo, upekuzi wa polisi katika klabu za usiku mjini Dar es Salaam ulilenga wanachama wa jamii ya LGBT, iliyoachiwa huru muda mfupi baadaye kwa kukosa ushahidi.

Katika mchakato huu, serikali ya Tanzania mpaka sasa imepiga marufuku uuagizaji na uuzaji wa mafuta ya kulainisha jeli, lakini muhimu kama nyongeza ya kudhibiti kinga dhidi ya maambukizi ya VVU.

Mnamo mwezi Februari, Waziri wa Afya aliamuru kufungwa kwa vituo vya afya arobaini, vinavyojihusisha na kupambana dhidi ya UKIMWI, vikituhumiwa kuendeleza ushoga. Uamuzi huu ulikosoa waziwazi na Marekani.

Naibu Waziri wa Afya wa Tanzania Hamisi Kingwangalla aliliambia bunge Ijumaa (Septemba 15) kwamba nchiya Tanzania itaendelea kupambana dhidi ya ushoga. "Tunapigana na nguvu zetu zote dhidi ya makundi yote yanayounga mkono ushoga katika nchi yetu," alihakikisha naibu waziri.

Idadi ya watu walioambukizwa VVU yaongezeka

Serikali ya Tanzania imeahidi pia katika miezi ya hivi karibuni kuwa wageni wanaotetea haki za mashoga watafukuzwa nchini.

Ukandamizaji huu kwa jina la maadili unatia wasiwasi mashirika ya kimataifa yanayojihusisha na afya. Ripoti ya hivi karibuni, iliyotolewa wiki iliyopita, inaarifu ongezeko kubwa la idadi ya watu walioathirika na virusi vya ukimwi nchini Tanzania, zaidi ya 35% katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Itakumbuka kwamba ushoga ni kinyume cha sheria katika nchini 38 kwa jumla ya 54 za Afrika na kitendo hicho kinasababisha adhabu ya kifo nchini Mauritania, Sudan na Somalia, kwa mujibu wa shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.