Pata taarifa kuu
RWANSA-UINGEREZA-UCHAGUZI-SIASA

William Gelling: Tuna wasiwasi na kukamatwa kwa wapinzani nchini Rwanda

Uingereza imekosoa vikali serikali ya Rwanda kwa kunyanyasa na kukamata wanasiasa wa upinzani tangu uchaguzi wa urais wa Agosti 4, ambapo rais anayemaliza muda wake Paul Kagame aliibuka msindi kwa 99% ya kura.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akisaini kiapo baada ya kuapishwa Ijumaa, Agosti 18 2017
Rais wa Rwanda Paul Kagame akisaini kiapo baada ya kuapishwa Ijumaa, Agosti 18 2017 Paul Kagame Twitter
Matangazo ya kibiashara

"Kuna hofu kuona viongozi wa upinzani wanalengwa, " almesema katika taarifa yake balozi wa Uingereza mjini Kigali, William Gelling.

"Nina wasiwasi kuhusu kukamatwa na matatizo ya kisheria ya wiki za hivi karibuni," Bw. Gelling ameongeza.

Mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara, ambaye alijaribu kugombea urais, kabla ya kuzuiwa na Tume ya Uchaguzi, alikamatwa na kuhojiwa na polisi kabla ya kuachiwa mapema mwezi Septemba.

Kwa mujibu wa polisi, familia yake iko chini ya uchunguzi ya ukwepaji wa kodi na inadiwa Dola milioni 5.9 (sawa na Euro milioni 5) na serikali, na Diane Rwigara anatuhumiwa kughushi hati katika jaribio lake la kuwania uchaguzi wa urais.

Lakini kwa mujibu wa watu walio karibu na mwanasuasa huyo wa upinzani, shutuma hizo hazina msingi na ni zina lengo la kumtisha.

Mmoja wa ndugu zake Diana, Aristide, ambaye anaishi nchini Marekani, anasema familia yake imekuwa toka wakati huo "chini ya ulinzi", madai ambayo polisi inakanusha.

Dada yake Diane, mama yake na ndugu wengine, "wanachukuliwa na kupelekwa kila asubuhi na polisi kuhojiwa na kurejeshwa nyumbani usiku wa manane," Bw. Aristide amesema.

Wiki iliyopita, viongozi saba wa vyama viwili vya Rwanda visivyotambuliwa na serikali, FDU-Inkingi kinachoongozwa na Victoire Ingabire, anayezuiliwa jela, walikamatwa.

Polisi inawatuhumu kuwa "uhusiano na makundi ya waasi yanayoendesha harakazi zao katika nchi jirani", ikimaanishwa Kundi la waasi wa Kihutu wa Rwanda la FDLR nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika taarifa yake, Bw Gelling pia amelezea wasiwasi wa serikali za Magharibi kuhusu jnsi uchaguzi wa urais ulivyofanyika nchini humo.

Amesikitishwa na "ukosefu wa uwazi katika mchakato wa kuandika"barua za wagombea, ambao ulizuia baadhi ya watu kujiandikisha, na pia baadhi ya "makosa katika kuhesabu matokeo."

Hata hivyo, Balozi wa Uingereza amekiri kuwa uchaguzi "unakwenda na nia ya idadi kubwa ya Wanyarwanda."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.