Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA

Marekebisho ya katiba yazua mjadala nchini Uganda

Hatua ya wabunge wa chama tawala nchini Uganda wa NRM kukubali kuidhinisha kufanyika kwa marekebisho ya katiba kuondoa kipengele cha ukomo wa umri wa rais imeibua mjadala miongoni mwa wananchi huku upinzani ukikosoa hatua hiyo.

Kwa upande wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, marekebisho ya Katiba ni muhimu.
Kwa upande wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, marekebisho ya Katiba ni muhimu. Capture d'écran al-Jazeera
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa wabunge wa NRM unamaanisha kuwa rais Yoweri Museveni atakuwa na uwezo wa kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao pamoja na chaguzi nyingine, ikiwa mswada huo uatapitushswa bungeni na katiba kufanyiwa marekebisho.

Upinzani unaona kuwa hatua ya wabunge wa NRM inalenga kumuongezea muda zaidi wa kukaa madarakani rais Museveni.

Itafahamika kwamba wabunge wa wote wa chama tawala NRM waliunga mkono azimio hilo lakini mbunge mmoja tu Monica Amoding ndiye aliyepinga uamuzi huo.

Uamuzi huu ulipingwa vikali na wanasiasa wa upinzani wakiongozwa na Kizza Besigye ambaye amekuwa mpinzani wa rais Yoweri Museveni kwa muda mrefu.

Uchaguzi ujao nchini Uganda ni mwaka 2021 kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo umri wa mwisho wa kugombea urais ni miaka 75. Rais Museveni atakuwa na umri wa miaka 76 wakati wa Uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.