Magavana watakiwa kukutana kwa mazungumzo na wauguzi wanaogoma
Chama cha wauguzi nchini Kenya kimeomba baraza la magavana kufikiria kufanya mazungumzo na wauguzi ambao wako kwenye mgomo kabla ya kuchukua hatua za kinidhamu.
Imechapishwa:
Hata hivyo wito wao unatolewa wakati huu mwenyekiti wa baraza la magavana Josphat Nanok akitupilia mbali uwezekano wowote wa kufanyika mazungumzo kati yao na wauguzi waliokataa kurejea kazini.
Kwenye taarifa yake gavana Nanok ameagiza uongozi wa hospitali ambazo wauguzi wake hawajarejea kazini kuwafuta kazi baada ya mahakama ya kazi kusema kuwa mgomo huo ulikuwa batili.
Wauguzi wa hospitali nchini Kenya wamekuwa kwenye mgomo toka mwezi juni mwaka huu ambapo wanashinikiza kupewa nyongeza ya mshahara na kulipwa marupurupu yao.