Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka

Emmerson Mnangagwa, aapishwa kuwa rais mpya wa Zimbabwe mbele ya maelfu ya raia wa nchi hiyo.

“ Mimi Emmerson Dambudzo Mnangagwa naapa kuwa rais wa Zimbabwe. Nitakuwa mwaminifu na kutii na kuilinda Katiba ya nchi,” alisema huku akishangiliwa....mengi zaidi hivi punde

E.A.C

Mgomo wa Wauguzi nchini Kenya wawalazimu wagonjwa kutafuta huduma Tanzania

media Wauguzi wanaogoma nchini Kenya wakishinikiza nyongeza ya mshahara na mazingira mazuri ya kufanya kazi www.coastweek.com

Wagonjwa kutoka Kaunti ya Taita Taveta na Kwale Pwani ya Kenya wanalazimika kuvuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Tanzania kupata huduma za afya kutokana na mgomo wa Wauguzi unaoendelea.

Huduma za afya zimekwama katika Hospitali mbalimbali za serikali Pwani ya Kenya na Kaunti zingine nchini humo kwa sababu wanataka kutekelezwa kwa mkataba wa kuwaongezea mshahara kama ilivyokubaliwa mwezi Machi.

Sekta ya afya nchini Kenya inashughulikiwa na serikali za Kaunti zinazosimamiwa na Magavana.

Wiki iliyopita, Baraza la Magavana nchini Kenya lilitoa wiki moja kwa Wauguzi hao kurudi kazini la sivyo watafutwa kazi.

Chama cha Wauguzi nchini humo kinasema kuwa wafanyikazi wake 25,000 wanaogoma hawatarudi kazini hadi pale matakwa yao yatakaposhughulikiwa.

Wanataka pia kuimarishwa kwa mazingira yao ya utendakazi.

Mgomo huu umekuwa ukiendelea tangu mapema mwezi Juni.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana