Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Kenyatta aapa kumuondoa Odinga madarakani akishinda

Wakati kampeni za uchauzi zikiendela nchini Kenya siku chache baada ya Mahakama ya Juu nchini humo kufuta matokeo ya uchaguzi, vitisho na maeneno makali vimeanza kusikika hapa na pale.

Wagombea wawili katika uchaguzi wa urais, Uhuru Kenyatta (kushoto) na mpinzani wake Raila Odinga.
Wagombea wawili katika uchaguzi wa urais, Uhuru Kenyatta (kushoto) na mpinzani wake Raila Odinga. TONY KARUMBA, SIMON MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema endapo raila Odinga atafanikiwa kushinda katika uchaguzi mpya ujao utakaofanyika mwezi Oktoba 17 yuko tayari kwa ushirikiano na chama chake kumuondoa madarakani muda mfupi baadaye kupitia bunge.

Uchaguzi mpya utafanyika tarehe 17 Oktoba baada ya matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti kufutiliwa mbali na Mahakama ya Juu.

Uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 8 ambapo rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi, ulifutwa na Mahakama ya Juu nchini humo kwa madai ya wizi wa kura.

Rais Kenyatta alikuwa ametangazwa mshindi akiwa na zaidi ya kura 1.4 milioni dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga lakini kiongozi huyo wa muungano wa National Super Alliance (NASA) alipinga ushindi wake mahakamani.

Kampeni zimekuwa zikishika kasi nchini humo viongozi wa chama Uhuru Kenyatta cha Jubelee na muungano wa NASA wakijibizana hasa kuhusu Tume ya Uchaguzi (IEBC) ambapo NASA wanataka tume hiyo ifanyiwe mabadiliko kwanza kabla ya uchaguzi kufanyika.

Kwa mujibu wa katiba nchini Kenya, Rais anaweza kuondolewa madarakani iwapo atabainika kutokuwa na uwezo kimwili na kiakili kuongoza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.