Pata taarifa kuu
TANZANIA

Mwanasiasa wa upinzani Tundu Lissu alazwa jijini Nairobi nchini Kenya

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu aliyepigwa risasi siku ya Alhamisi mjini Dodoma, amelazwa katika Hospital ya Aga Khan jijini Nairobi.

Hospitali ya Agakhan jijini Nairobi
Hospitali ya Agakhan jijini Nairobi agakhanhospitals.org
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria nchini Kenya LSK Isaac Okero amethibitisha hilo na kusema Lissu aliwasili jijini Nairobi Alhamisi usiku.

Aidha, amesema kuwa Mawakili wa Chama cha wanasheria cha Afrika Mashariki watamtembelea Lissu Ijumaa mchana. Wamelaani shambulizi hilo.

“Tumeelezwa kuwa hali yake bado ni mbaya,” amesema Okero.

Tundu Lissu pia ni rais wa Chama cha Mawakili cha Tanganyika na mwanasheria Mkuu wa chama chake cha CHADEMA.

Wanasiasa wa upinzani, chama tawala nchini humo CCM na rais John Magufuli wamelaani tukio hilo na kutaka maafisa wa usalama kufanya uchunguzi kuwabaini waliohusika na kuwafungulia mashtaka.

Ripoti zinasema kuwa Lissu alipigwa risasi tumboni, mgongoni na mguuni akiwa ndani ya gari lake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.