Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

IEBC kwa Jubilee na NASA: Tuko huru hatupangiwi cha kufanya

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Wafula Chebukati amesema Tume hiyo ni huru na hivyo haiwezi kuchukua maagizo kutoka kwa mtu mwingine kuhusu maandalizi mapya ya Uchaguzi mwezi Oktoba.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Wafula Chebukati
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Wafula Chebukati IEBCKenya
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya chama cha Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta na muungano wa upinzani NASA, kuiandikia barua Tume hiyo kupinga watendaji wapya waliotangazwa na Mwenyekiti Chebukati siku ya Jumanne usiku.

Chebukati ameiandikia barua NASA na Jubilee na kuwaambia kuwa, Tume hiyo ina uwezo wa kufanya mabadiliko kwa watendaji wao kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo kifungu cha 249.

NASA, inataka baadhi ya wafanyikazi wa Tume hiyo waachishwa kazi akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Ezra Chiloba.

Chama cha Jubilee nacho kinasema mabadiliko yaliyofanyika hayakubaliki kwa sababu, watendaji hao wapya wanaegemea mrengo wa kisiasa.

Tume hiyo imetangaza kuwa Uchaguzi wa marudio  ya urais utafanyika tarehe 17 mwezi Oktoba.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.