Pata taarifa kuu
EAC-KISWAHILI

Baraza la Kiswahili la Jumuiya ya Afrika Mashariki lazinduliwa

Tume ya Lugha ya Kiswahili ya Afrika Masharik imezinduliwa rasmi kwa kwa lengo la kuhimiza uzungumzaji wa lugha hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki yenye watu zaidi ya Milioni 150.

Makamuwa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizundua Tume ya lugha ya Kiswahili ya Afrika Mashariki
Makamuwa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizundua Tume ya lugha ya Kiswahili ya Afrika Mashariki kiswacom.org
Matangazo ya kibiashara

Akizindua Tume hiyo visiwani Zanzibar, Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Tume hiyo itasaidia kuinua maendeleo na ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha, amesema kuwa lugha ya Kiswahili ikitumiwa vema ina uwezo mkubwa wa kuwaunganisha wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwa kitu kimoja.

Tanzania imesema itaendelea kushirikiana na Mataifa mengine ya Afrika Mashariki kuhimiza na kuinua uzungumzaji wa lugha ya Kiswahili.

Kiswahili, kimesaidia wafanyibiashara kuendeleza shughuli za kiuchumi na kurahihisha mawasiliano kati ya nchi wananchi.

Nchi zinazozungumza lugha ya Kiswahili ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Kiswahili ni lugha ya taifa nchini Tanzania na Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.