Pata taarifa kuu
BURUNDI-UN-HAKI

Tume ya Umoja wa Mataifa yatoa ripoti yake kuhusu uhalifu nchini Burundi

Tume huru ya uchunguzi kuhusu uhalifu uliofanywa nchini Burundi ilitoa ripoti yake siku ya Jumatatu (Septemba 4). tume hiyo imeomba Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuchunguza kwa dharura, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu mwingine uliofanywa nchini Burundi.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza hakutajwa kwa jina lake, lakini ripoti hii inaelezea kuhusu mchango wake katika uhalifu huo uliofanywa nchini Burundi.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza hakutajwa kwa jina lake, lakini ripoti hii inaelezea kuhusu mchango wake katika uhalifu huo uliofanywa nchini Burundi. REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa tume hiyo amesema "mashambulizi yaliyowalenga kwa pamoja" raia wa kawaida yalishuhudiwa nchini Burundi. Fatsah Ouguergouz amesema mpango huo uliandaliwa na kutekelezwa na serikali. Ripoti hiyo inasema uhalifu huo ulitekelezwa na viongozi kuanzia ngazi ya juu serikalini hadi kuendelea. Hii ni mara ya kwanza ripoti ya tume huru ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kushtumu viongozi kuanzia ngazi ya juu serikalini.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza hakutajwa kwa jina lake, lakini ripoti hii inaelezea kuhusu mchango wake katika uhalifu huo uliofanywa nchini Burundi.

Kwa mujibu wa ripot hii, uhalifu mkubwa kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu ulioandaliwa na makundi mbalimbali yanayoungwa mkono na utawala wa sasa wa Burundi. Makundi haya ni pamoja na Idara ya taifa ya ujasusi, polisi, vitengo vya jeshi, na Imbonerakure, vijana wa chama tawala ambao Umoja wa Mataifa unawaita wanamgambo.

Maamuzi yalichukuliwa "sio na serikali bali na rais Pierre Nkurunziza akizungukwa na kundi lake dogo la maafisa watano wa jeshi wa ngazi ya juu, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Usalama na Katibu Mkuu wa Chama cha Nkurunziza.

Mshauri Mkuu wa rais Nkurunziza katika masuala ya mawasiliano Willy Nyamitwe alijibu akisema kuwa hizo ni njama za nchi za Magharibi dhidi ya Nkurunziza, "kwa sababu ni mtu muhimu katika ulinzi wa taifa. Ni mhusika mkuu anaelengwa na jama hizo za nchi za magharibi, " amesema Bw Nyamitwe.

Mashirika ya kiraia ya Burundi yalio uhamishoni yamekataa kuhusika kwao katika ukandamizaji unaoendelea kushuhudiwa nchini Burundi. Yameelezea furaha yao kuona Pierre Nkurunziza akihusishwa kwa uhalifu huo kwa mara ya kwanza. Na yameiomba ICC kuwafungulia mashitaka wahalifu wa uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanywa Burundi kwa zaidi ya miaka miwili, bila kujali cheo chao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.