Pata taarifa kuu
RWANDA-UCHAGUZI-HAKI

Polisi Rwanda: Rwigara na familia yake wanahojiwa

Polisi nchini Rwanda, imekanusha taarifa zilizozagaa mitandaoni kwamba mpinzani wa rais serikali Diane Rwigara na familia yake hawajulikani walipo muda mfupi baada ya kukamatwa na polisi.

Diane Rwigara (kushoto) anahojiwa kwa tuhuma zinazomkabili, kwa mujibu wa polisi ya Rwanda.
Diane Rwigara (kushoto) anahojiwa kwa tuhuma zinazomkabili, kwa mujibu wa polisi ya Rwanda. CYRIL NDEGEYA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu septemba 4, polisi nchini humo imewashikilia Diane Rwigara na watu wengine wawili wa familia yake akiwemo mama yake katika kile kilichoelezwa kwamba ni kwa sababu za uchunguzi.

Kupitia mkanda wa video unaotembea kwenye mtandao wa Internet, Diane Rwigara anaonekana akiwa na ndugu zake huku kukiwa na majibizano na polisi akiwatuhumu kuwapora pesa na simu akilaumu kwamba polisi imewafungia ndani huku ikitaka waripoti kituoni.

Hata hivyo msemaji wa polisi nchini Rwanda ACP Theos Badege amesema walichokifanya ni kutekeleza sheria.

Hadi sasa imekuwa vigumu kuelewa nini kilichotokea siku nne zilipo baada ya kuzagaa za taarifa za kutoweka kwa mpinzani huyo ambae anatuhumiwa kutumia nyaraka bandia wakati akiwasilisha fomu za kuwania uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.