Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Burundi yafutlia mbali ripoti ya tume ya Umoja wa Mataifa

media Maiti ya mtu asiejulikana katika moja ya mitaa ya mji wa Bujumbura, Desemba 12, 2015. REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimana

Serikali ya Burundi imetupilia mbali yaliomo katika ripoti iliotolewa jana na tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu ilioeleza bayana kuhusu mauaji yaliotokea nchini humo tangu mwaka 2015.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamewasilisha ripoti hapo jana mbele ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuthibitisha uwepo wa mauaji ya kivita nchini Burundi hivyo tume hiyo ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wameitaka mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC kuanzisha uchunguzi haraka iwezekanavyo kabla ya October 16.

Mwenyekiti wa tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi Fatsah Ouguergouz amesema mashambulizi yanalengwa hasa kwa wapinzani wa serikali na wale wote walioshiriki katika maandamano ya kupinga muhula wa 3, wakiwemo pia wanaharakati wa mashirika ya kiraia, pamoja na waandishi wa habari.

Hata hivyo orodha ya siri iliowalishwa kwenye tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inawalenga hasa vijana wa chama tawala imbonerakure, pamoja na viongozi mbalimbali wa kijeshi polisi na idara ya ujasusi pamoja na watu wa karibu na rais Pierre Nkurunziza.

Waziri wa haki za binadamu Martin Nivyabandi ameitaka tume hiyo ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuwasilisha orodha hiyo ili wahusika waadhibiwe nchini Burundi, na kwamba  "Tumeomba kupewa majina hayo mnayosema kwamba ndio wahusika wa mauaji ili tuweze kuwapa mwanga wa nini kilichotokea nchini kwetu ni kina nani wahusika na nani hawakuhusika, vinginevyo vyombo vya sheria vipo tayari kuwahukumu wataohusika. lakini hadi sasa tunaelezwa tu kwamba ni viongozi wa serikali, kwa upande wetu bado ni mapema mno kuzungumzia watu tusiowafahamu, watu ambao hawakutajwa na tume hiyo, lakini pia, lazima uchunguzi ufanyike, ili kutoa mwanga kuhusu kila tukio, kila jina, kila mtu ili tutoe mwanga, lakini hatukupewa haki ya kufahamu majina ambayo hadi sasa yamesalia kuwa siri."

Serikali ya Burundi ilitangaza kujiondoa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kvita ya ICC ambapo hadi Octoba mwaka huu itakuwa sio mwanachama tena.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana