Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Odinga amshutumu rais Kenyatta, ataka Tume ya Uchaguzi kufanyiwa marekebisho

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, unataka mabadiliko kufanyika ndani ya Tume ya Uchaguzi kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi mpya wa urais.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga akikutana na wafuasi wake jijini Nairobi
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga akikutana na wafuasi wake jijini Nairobi REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kenya inaelekea kwenye Uchaguzi mpya ndani ya siku 60 baada ya Mahakama ya Juu kufuta ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kwa kubaini kuwa, haukuwa huru na haki.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, amesema Tume ya Uchaguzi haiaminiki na haiwezi kusimamia Uchaguzi utakaokuwa huru na haki kama Mahakama Kuu ilivyoagiza.

Kauli ya Odinga imekuja baada ya kuanza kampeni zao za kwanza jijini Nairobi siku ya Jumapili kutokana na uamuzi huo wa Mahakama Ijumaa iliyopita.

Aidha, Odinga amekosoa kauli ya rais Kenyatta ya kuwashtumu Majaji lakini pia kudai kuwa upinzani hawataki Uchaguzi lakini wanataka serikali ya muungano, madai ambayo Odinga amepuuzilia mbali na kusema hawawezi kushirikiana na wezi wa kura.

Rais Kenyatta na wanasiasa wa Jubilee wamekasirikishwa na uamuzi wa Mahakama ya Juu na kuonya kuwa ikiwa watachaguliwa tena, watairekebisha Mahakama hiyo.

Kenya imekuwa nchi ya kwanza, barani Afrika kufuta Uchaguzi wa urais na kuingia katika vitabu vya historia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.