Pata taarifa kuu
KENYA-MAHAKAMA-SIASA

Upinzani nchini Kenya washerehekea uamuzi wa Mahakama ya Juu

Viongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, wameipongeza Mahakama ya Juu nchini humo kwa kufuta ushindi wa rais Uhuru Kenyatta.

Wafuasi wa kiongozi wa upinzani nchini Kenya wakisherehekea jijini Nairobi baada Mahakama kufuta ushindi wa rais Uhuru Kenyatta
Wafuasi wa kiongozi wa upinzani nchini Kenya wakisherehekea jijini Nairobi baada Mahakama kufuta ushindi wa rais Uhuru Kenyatta REUTERS/ Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa NASA Raila Odinga, akizungumza muda mfupi baada ya uamuzi huo katika Mahakama ya Juu jijini Nairobi, alisema uamuzi huo ni wa kihistoria kwa raia wa Kenya na bara la Afrika.

“Huu ni ushindi kwa wananchi wa Kenya na bara la Afrika,” alisema Odinga akionekana mwenye furaha na mchangamfu.

Aidha, amesema kuwa imekuwa ni siku ya kihistoria na ya mara ya kwanza barani Afrika kwa sababu barani Afrika, hakuna Mahakama ambayo imewahi kufuta ushindi wa rais barani Afrika.

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga akisherehekea uamuzi wa Mahakama jijini Nairobi
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga akisherehekea uamuzi wa Mahakama jijini Nairobi REUTERS/Baz Ratner

Mbali na hilo, Odinga amesema kuwa wao kama wapinzani hawana imani na Tume ya Uchaguzi na hivyo hawawezi kwenda katika Uchaguzi huo.

Odinga pia amesema awafungulia Mashataka Makamishena wa Tume ya Uchaguzi kwa kusababisha wizi wa kura katika Uchaguzi uliopita.

Wito kama huo umetolewa na aliyekuwa mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka ambaye amesema uamuzi wa Mahakama ya Juu ni wa kihistoria.

“Leo nafurahi kuwa raia wa Kenya,” amesema Kalonzo.

Musyoka pia amesifu ujasiri wa Mahakama na kusema utabadilisha mustakabali wa siasa nchini Kenya katika siku zijazo.

Wachambuzi wa siasa nchini Kenya wanasema kuwa, uamuzi huu umeleta imani kubwa kwa idara ya Mahakama nchini humo kinyume na ilivyokuwa mwaka 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.