Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI-MAHAKAMA

Rais Kenyatta: Sikubaliani na uamuzi wa Mahakama lakini nauheshimu

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema hakubaliani na uamuzi wa Mahakama ya Juu lakini anauheshimu, baada ya ushindi wake wa mwezi Agosti kufutwa.

Uhuru Kenyatta akizungumza na wafuasi wake jijini Nairobi Septemba 1 2017
Uhuru Kenyatta akizungumza na wafuasi wake jijini Nairobi Septemba 1 2017 REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kenyatta amesema maamuzi ya Wakenya yamekataliwa na watu ambao amesema ni watu sita, ambao walikuwa ni Majaji wa Mahakama hiyo ya Juu.

Aidha, Kenyatta amesema kuwa yuko tayari kurejea tena kwenda kuomba kura kwa wananchi na kumenyana na mpinzani wake Raila Odinga.

Pamoja na hilo, amewataka Wakenya kuendelea kuwa watulivu wakati huu Uchaguzi mpya ukipangwa.

Wakati uo huo, Tume ya Uchaguzi imesema kuwa imekubali uamuzi wa Mahakama na itaanza mikakati ya kupanga Uchaguzi mpya baada ya kupata uamuzi kamili.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati amesema kuwa wale watakaopatikana walihusika na kosa hilo, watafunguliwa mashtaka.

Hata hivyo, amesema kuwa hatajiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.