Pata taarifa kuu
RWANDA-SIASA-USALAMA

Hatma ya mpinzani wa Paul Kagame mashakani

Polisi nchini Rwanda imeendelea kuwa kwenye shinikizo zaidi kutoka kwa familia ya aliyekuwa mmoja wa waliotaka kuwania kiti cha urais nchini humo Diane Rwigara anayedaiwa kushikiliwa na vyombo vya usalama.

Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda, mmoja wa waliotaka kuwania kiti cha urais nchini humo Diane Rwigara.
Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda, mmoja wa waliotaka kuwania kiti cha urais nchini humo Diane Rwigara. REUTERS/Jean Bizimana
Matangazo ya kibiashara

Taarifa mpya kutoka ndani ya familia yake zinasema kuwa mwanamama Diane Rwigara na ndugu wengine watano wa familia hiyo wanashikiliwa na vyombo vya usalama wakikanusha taarifa za awali zilizotolewa na polisi kuwa hajakamatwa.

Katika matangazo yetu ya juma hili tuliripoti kuhusu taarifa za kukamatwa kwa Diane, taarifa ambazo hata hivyo zilikanushwa vikali na polisi wa Rwanda ambao walikiri kumchunguza lakini wakasisitiza hayuko kwenye mikono yao.

Hata hivyo kaka yake Diane amesititiza dada yake kuchukuliwa na polisi nyumbani kwake Jumanne ya wiki hii ambapo ameitaka polisi kueleza ukweli kuhusu mahali alipo dada yao.

Hivi karibuni tume ya uchaguzi ilidai kuwa Diane aliwasilisha nyaraka za kughushi wakati alipokuwa anataka kuwania kiti cha urais, madai ambayo Diane mwenye aliyakanusha.

Katika hatua nyingine kampuni ya tumbaku inayomilikiwa na familia yake pia imeeleza kuwa chini ya uchunguzi kwa madai ya ukwepaji kodi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.