Pata taarifa kuu
KENYA-MAHAKAMA-ODINGA-KENYATTA

Kesi ya kupinga matokeo ya urais nchini Kenya: Fahamu mambo muhimu

Mahakama ya Juu nchini Kenya wiki hii ilisikiliza kesi ya kupinga ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kwa siku mbili jijini Nairobi.

Majaji wa Mahakama ya Juu nchini Kenya, wiki hii
Majaji wa Mahakama ya Juu nchini Kenya, wiki hii www.judiciary.go.ke
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo iliwasilishwa na kiongozi wa Muungano wa upinzani NASA, Raila Odinga baada ya kukataa matokeo yaliyompa ushindi rais Kenyatta baada ya zoezi hilo la tarehe nane mwezi Agosti.

Siku ya Ijumaa, Mahakama itatoa uamuzi. Inaweza kuamua kuwa ushindi wa Kenyatta haukuwa halali au matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi yalikuwa halali.

-Uchaguzi ulifanyikaje ?-

Wakenya walijitokeza kwa wingi kupiga kura, huku Tume ya Uchaguzi ikisema kuwa wapiga kura Milioni 15.5 kati ya Milioni 19 waliojiandikisha, ndio waliopiga kura.

Waangalizi wa Kimataifa walisema kuwa zoezi hilo lilifanyika vema na kwa amani hali iliyowapa wapiga kura nafasi ya kutekeleza haki yao ya kikatiba.

Agosti 11 Tume ya Uchaguzi IEBC ilimtangaza Uhuru Kenyatta mshindi kwa kupata asilimia 54.27 huku Raila Odinga akiwa wa pili kwa asilimia 44.74.

Odinga alikataa kuyamtambua matokeo hayo, hal iliyozua maandamano ya wafuasi wa upinzani mjini Kisumu, mtaani Mathare na Kibera jijini Nairobi na kusababisha vifo vya watu 21, akiwemo mtoto mchanga na msichana wa miaka tisa.

-Upinzani wanataka nini ? -

Muungano wa upinzani NASA, unataka Mahakama kutupilia mbali matokeo yaliyompa ushindi rais Uhuru Kenyatta na kuitisha Uchaguzi mpya ndani ya siku sitini.

Kuthibitisha hili, Mawakili wa upinzani waliiambia Mahakama kuwa Tume ya Uchaguzi ilighushi matokeo yaliyompa Kenyatta ushindi katika fomu za 34 A na 34 B.

Majaji wa Mahakama ya Juu waliagiza kuwa upinzani upewe nafasi ya kuangalia mitambo ya IEBC iliyokuwa na matokeo halisi, lakini James Orengo wakili wa upinzani akasema kuwa hawakupewa nafasi ya kuangalia mitambo hiyo.

Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi ilikanusha madai hayo ya upinzani na kujitetea kuwa matokeo waliyotangaza ndiyo yaliyokuwa sahihi kutoka vituo vya kupigia kura.

Majaji walipokea ripoti tofauti zinazokinzana kuhusu zoezi la kuhakiki mitambo ya IEBC.

-Matarajio kuhusu kesi hii ? -

Mahakama ya Juu itaamua kufutilia mbali matokeo hayo au kuyathibitisha.

Ikiwa yatatupiliwa mbali, Uchaguzi mwingine utafanyika baada ya siku 60 lakini ikiwa itayathibitisha, Uhuru Kenyatta ataapishwa baada ya wiki moja ili kuhudumu kwa muhula wa pili na wa mwisho.

Mwaka 2013, kulikuwa na kesi kama hii lakini ikafutiliwa mbali katika mazingira ambayo hayakuwafurahisha watu wengi, baada ya ushindi wa Odinga kutokubaliwa Mahakamani.

Wachambuzi wa siasa wanaona kuwa, kwa namna yeyote ile ambayo uamuzi utatolewa, utazua hofu nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.