Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Kesi ya kupinga ushindi wa Kenyatta kusikilizwa jumapili mchana

Kesi ambayo kiongozi wa Upinzani nchini Kenya Raila Odinga anapinga kuchaguliwa tena kwa rais Uhuru Kenyatta, itaanza kusikilizwa rasmi jumapili saa tisa mchana na kuendelea hadi Tarehe moja mwezi ujao ambapo majaji saba watatoa uamuzi wao.

Raisi Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto
Raisi Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto rfi
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo ilianza jumamosi kwa maelezo ya mwanzo ambayo kila upande ulitoa ili kuhakikisha nafasi kwa kusikilizwa rasmi.

Katika kikao cha kwanza ambacho kilichukua muda wa masaa matano, na kumalizika saa tano usiku,mawakili wa pande zote walitoa maombi yao  na matakwa yao ya kisheria.

Ombi kuu alilotoa James Orengo, mmoja wa mawakili wa Raila Odinga lilikuwa mahakama kumruhusu kumulikwa kwa mitambo ya kompyuta ambayo imehifadhi hati rasmi za uchgaguzi uliofanywa mapema mwezi huu.

Hata hivyo ombi la Orengo lilipingwa vikali na mawakili wanaomwakilisha rais Uhuru Kenyatta na pia tume inayosimamia uchaguzi Kenya.

Majaji wa mahakama hayo ya juu Kenya wanatarajiwa kutoa uamuzi wao saa nane leo mchana ikiwa watamruhusu ama kukataa ombi la wakili Orengo, kumulika kompyuta inayohifadhi hati za uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.