Pata taarifa kuu
TANZANIA

Tanzania yaipa UNHCR siku 7 kuwarejesha kwa hiari wakimbizi wa Burundi

Serikali ya Tanzania imetoa siku saba kwa shirika la wakimbizi duniani UNHCR kuanza kuwarudisha wakimbizi wa Burundi ambao wanataka kurudi kwao kwa hiari, ama sivyo serikali yenyewe itafanya zoezi hilo.

Wakimbizi wa Burundi
Wakimbizi wa Burundi rfikiswahili/Abuso
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Mwigulu Nchemba ametoa agizo hilo siku ya Alhamisi alipokuwa katika ziara ya kikazi katika kambi ya Nduta Magharibi mwa Tanzania ambayo ni moja ya kambi zinazohifadhi wakimbizi wengi wa Burundi.

Waziri Nchemba amewashutumu maafisa wa UNHCR kwa kuchelewesha zoezi hilo la kuwarudisha nyumbani wakimbizi wa Burundi wanaotaka kurejea nchini kwao kwa hiari.

Tanzania ndio nchi inayoongoza Afrika Mashariki kwa kuhifadhi wakimbizi wengi kutoka Burundi.

Zaidi ya wakimbizi elfu 8 kati ya laki moja ishirini na sita elfu katika kambi ya Nduta, ambayo Waziri Nchemba aliitembelea, wanasemekana kuwa wamejiandikisha kurejea kwao Burundi kwa hiari.

Hata hivyo UNHCR inasema wanataka kujiridhishia kwamba hali ya usalama nchini Burundi inaridhisha kabla haijaanza kuwarudisha wakimbizi hao.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.